Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Hassan Rouhani alisema hayo jana Jumanne katika kikao cha Kamati ya Uratibu wa Kiuchumi ya Serikali ya Iran. Ameashiria nguvu na uwezo mkubwa wa kiuchumi wa Iran na kusema, ijapokuwa vita vya kiuchumi vilivyoanzishwa na Marekani vimesababisha madhara na na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na katika maisha ya wananchi, lakini leo hii walioweka vikwazo na wanaopiga ngoma ya vita ambao walitaraji kuona uchumi wa Iran unasambaratika haraka sana, wanaondoka katika Ikulu ya Marekani White House huku taifa la Iran likiwa imara na likijifakharisha kwa ushindi wake katika vita hivyo ilivyobebeshwa kidhalimu bila ya mlingano sawa.
Amesema, muqawama na kusimama kidete taifa la Iran mbele ya mashinikizo na vita vikubwa vya kiuchumi vya pande zote vilivyoanzishwa na Donald Trump dhidi ya Tehran, kumewadhihirishia kivitendo walimwengu na maadui wote uhakika wa taifa hili la Kiislamu.
Ameongeza kuwa, Trump hakujua kabisa uwezo, nguvu na wala uhakika wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na alichukua hatua zake za kiuadui kwa kutegemea ndoto zake za alinacha.
Rais Rouhani vile vile amesema, kufeli Marekani katika siasa zake za kukabiliana na Iran baada ya miaka miwili na nusu ya vita vyake vya pande zote dhidi ya taifa hili pamoja na kushindwa siasa za White House kimataifa, ndiko kulikombwaga Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani.
342/